Bryba ni msanii wa kuimba kutoka mji wa Watamu katika kaunti ya Kilifi.

Safari ya msanii Bryba katika ulingo wa sanaa ya kuimba ilianza tu baada ya kumaliza masomo ya shule ya upili mwaka wa 2013. Tangu hapo ameweza kufanya kazi kadhaa ikiwemo video moja.

Mapenzi ya mziki

Bryba anadai chimbuko lake la mziki lilianza akiwa shuleni. Marafiki wake wa shule na machizi  mtaani ndio waliokuwa sababu kubwa yake kuingia ndani ya sanaa ya mziki. Hii ilimfanya kuanza kuimba  shuleni na wakati wowote anapata akiwa mtaani.

BrybaMentor wa Bryba katika muziki

Bryba ametilia mkazo sana nafasi iliyochezwa na Sudi boy katika maisha yake na vile vile safari yake ya mziki. Anadai kuwa Sudi Boy amekuwa “Role model” wake na pia mentor ni Sudi Boy huku akicheza nafasi kubwa katika safari iliyomfikisha pale alipo sasa.

Mchango wa Sanaa katika Maisha

Sanaa imemfika alipo sasa na anasema kika siku anazidi kukua kama msanii ila changamoto zipo kibao. Changamoto kubwa ni kipato kidogo cha hela. Anakiri kuwa kila  kitu kinazukia pesa na bila huwezi fanya kitu. Hili halijamfanya Bryba apunguze bidii katika kazi ilo ili awaze kufanisha malengo

Matarajio kwa Mashabiki?
Anataka mashabiki wake watarajie video kadhaa mwaka huu. Vile vile anaahidi collabo chungu mzima (amebana majina ya kazi hizo na wale ambao atawashirikisha). Lakini kazi hizi zitamfanya apande katika anga ya mziki.

Summary
Photo ofBryant Baraka
Name
Bryant Baraka
Nickname
(Bryba)
Job Title
Musician
Address
Watamu Road,
Malindi, Kilifi County, 80200